• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MACHA AMKABIDHI KITIMWENDO MTOTO MWENYE ULEMAVU (ESTER MAIKO) KILICHOTOLEWA NA MHE. KATAMBI NA TZS. 300,000/= KUTOKA KWA MHE. CHRISTINA MZAVA MBUNGE WA MKOA WA SHINYANGA.

Posted on: March 16th, 2025

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amemkabidhi Kitimwendo na Tzs. 300,000/= (Laki tatu) mtoto Ester Maiko ambaye ni mwenye ulemavu wa viungo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Mhe. Patrobas Katambi Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini pamoja na Mhe. Christina Mzava ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga wakati wa Kongamano la Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) wakiadhimisha Siku ya Wanawake na Wanawake wenye ulemavu, ili kiweze kumsaidia mtoto na mzazi wake aweze kufanya biashara ndogondogo ambayo itamuwezesha kujikimu kwa namna moja au nyingine.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, RC Macha alimshukuru sana Mhe. Katambi na Mhe. Christina kwa namna ambavyo waliweza kuguswa, kujitolea na kumsaidia mtoto Ester na mzazi wake katika uhitaji wao huku akiwapongeza (SMAUJATA) ngazi zote kwa kuweza kufuatilia, kuibua na kusimamia mambo mbalimbali likiwemo hili la mtoto Ester pamoja na mambo yote yanayohusu mapambano dhidi ya ukatili wa aina yoyote ile kwa jamii zetu.

"Kwa dhati kabisa, ninamshukuru sana Mhe. Katambi kwa kutoa kitimwendo na Mhe. Christina kwa kutoa fedha Tzs. 300,000/= (laki tatu) kwa mzazi wa ambazo zitamsaidia kufanya shughuli ndogondogo za kujikwamua kimaisha changamoto ambayo iliibuliwa na SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga katika Kongamano la Siku ya Wanawake na Wanawake wenye Ulemavu, na kipekee pia niwapongeze SMAUJATA kwa kazi nzuri mnayoendelea nayo ya kuihudumia, kuipambania na kuisogelea jamii yetu," alisema RC Macha.

Ikumbukwe kwamba, mnamo tarehe 1 Machi, 2025 kulifanyika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga katika ukumbi wa Lyakale Manispaa ya Shinyanga ambapo uwepo wa mtoto Ester na changamoto yake iliyokuwa na uhitaji wa kitimwendo na msaada zaidi iliyoibuliwa na SMAUJATA kwa lengo la kumsaidia na ndipo ahadi za Waheshimiwa Wabunge zilitolewa na leo zimetekelezwa kwa vitendo.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa