Na. SHINYANGA RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewakaribisha Viongozi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Binilith Mahenge ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia amewaeleza juu uwepo na umuhimu wa Kongani la Biashara Buzwagi - Kahama ambapo ni eneo kubwa sana na maalum la Uwekezaji wa Viwanda.
Pia Shinyanga inayo maeneo makubwa sana ya uwekezaji, rasilimali vitu, watu na miundombinu yote muhimu ipo ikiwa ni pamoja na barabara, reli, uwanja wa ndege ambao unakajkoika hivi karibuni, maji, umeme nk.
Macha amebainisha hayo wakati akizungumza na viongozi hao ofisini kwake ambao pamoja na Dkt. Mahenge, pia ameambatana na Felix John Meneja Uhamasishaji Uwekezaji wa ndani pamoja na Phina Jerome ambaye ni Meneja TIC Kanda ya Ziwa.
"Tunawakaribisha sana hapa mkoani Shinyanga viongozi kutoka TIC, mkiwa hapa mtapata wasaa wa kutembelea Kiwanda cha Jielong Holding (T) LTD kilichpo Manispaa ya Shinyanga na Msumba Steel Co. LTD cha Manispaa ya Kahama kama mlivyopendekeza," amesema RC Macha.
Akitoa salamu za Bodi, Dkt. Mahenge amesema kuwa wamekuja Shinyanga kuangalia kama waliyokubaliana katika usajili wa miradi yanatekelezwa, kusikiliza na kutatua changamoto, kuhamasisha uwekezaji huku akimpongeza RC Macha kwa Mkoa wa Shinyanga ambao umesajili miradi 901 yenye thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekeni Bil 1.6.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa