RC MACHA KUZINDUA KAMPENI YA CHANJO DHIDI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
Ni tarehe 22 Aprili, 2024 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ndala 'A' Manispaa ya Shinyanga na muda ni saa 3:00 asubuhi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Kampeni hii ya Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi.
Kuanzia tarehe 22 Aprili hadi 28, 2024 itakuwa ni Wiki ya Chanjo, ambapo walengwa wa zoezi hili ni wasichana wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14, ambapo baada ya uzinduzi huu chanjo hii itakuwa ikitolewa katika shule zote za Msingi na Sekondari hapa Mkoani Shinyanga
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi wote Mkoani Shinyanga kuhakikisha kuwa wanawaruhusu watoto wao kuja kupata chanjo hii muhimu na isiyokuwa na madhara yoyote.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa