Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 9 Agosti, 2023 amefungua kikao cha tathimini ya lishe Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na maelekezo mengine lakini pia ameziagiza Halmashauri zote Mkoani Shinyanga kutilia mkazo wa siku ya usafi kitaifa ambapo kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi huadhimishwa kwa kufanya usafi huku akiwataka kuwa wanaitangaza siku hiyo kwa kwa kuwakumbusha wananchi waweze kushiriki kikamilifu.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo mbele ya wajumbe wa lishe mkoa ambao walipata wasaa wa kuwasilisha taarifa kutoka katika kila Wilaya zao ambapo kwa ujumla ilionesha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ni nzuri sana kwakuwa zimekuwa na alama nzuri zote.
"Leo tupo hapa kwa ajili kufanya kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe mkoani kwetu ambapo kwa ujumla hali ipo vizuri sana, lakini jambo moja muhimu sana la kuzingatia ni kuwekea mkazo siku ya usafi wa mazingira ambapo kila jumamosi ya mwisho wa mwezi wananchi washirikishwe kufanya usafi kwa dhati kabisa na wawe wanakumbushwa kwa matangazo," alisema Mhe. Mndeme.
Kando na hayo, Mhe. Mndeme alisisitiza juu ya kutengwa kwa Tzs. 1000 kwa kila mtoto ambapo itatekelezwa kwenye afua za lishe jambo ambalo litaimatisha zaidi afya zao.
Aidha alielekeza Vijiji na Mitaaa yote Mkoani Shinyanga kufanya Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ili elimu iweze kuwafikia wananchi wote, pia Halmashauri zote hapa Shinyanga zitumie vikao vyote vya kikanuni kuweka ajenda ya lishe ili iweze kujadiliwa ambapo watafanya tathimini ya wapi wamefikia na wapi wamekwama waweze kuboresha na kisha akawaagiza Afisa Lishe wote ndani ya Mkoa wa Shinyanga waende kwa wananchi kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara wasikae ofisini.
"Katika hili, naelekeza afisa lishe wote kwenda kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao ambapo mtafanya mikutano na hapo ndiyo mtaweza kutoa elimu kwa wananchi wetu, msikae ofisini nendeni kwa wanananchi mkaifanye kazi hii naagiza," alisisitiza Mhe. Mndeme
Katika hatua nyingine Mhe. Mndeme amewapongeza sana waandishi wa habari wote Mkoani Shinyanga kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhabarisha na kutoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na nje ya mkoa pia, jambo ambalo limepelekea jamii kuelimika sana na hivyo kusaidia kuimarisha afya zao, usafi wa mazingira na kupendezesha miji sambamba na kuelimisha umma juu ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita kwa wananchi wake.
PICHA NA MATUKIO BAADA YA KIKAO
Picha ikionesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mndeme akikabishi zawadi kwa mshindi wa usafi na utunzaji wa mazingira kwa Halmashauri 6 za mkoa ambapo Manispaa ya Shinyanga waliibuka mshindi namba moja
@ortamisemi @christinamndeme18
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa