RC MNDEME APOKEA NA KUKABIDHI MIPIRA 1000 KWA HALMASHAURI ZA MKOA WA SHINYANGA
Na. Shinyanga RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amepokea mipira 1000 kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF) na kukabidhi kwa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga huku akizielekeza kwenda kutumia mipira hii kwa lengo lililokusudiwa ikiwemo kukuza vipaji kwa vijana, kuimarisha michezo na kuibua vipaji vipya
Makabidhiano haya yamefanyika tarehe 28 Feb, 2024 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo pamoja na maelekezo hayo kupitia kwa Maafisa Michezo wa Halmashauri, RC MNDEME ameipongeza sana na kuishukuru TFF kwa kuupatia Mkoa mipira hii.
"Pamoja na shukrani nyingi kwa TFF lakini nizielekeze Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga, kwenda kutumia mipira hii kwa lengo lililokusudiwa na siyo vinginevyo", amesema RC MNDEME.
Aidha, amewataka walimu wa michezo kutoiweka Stoo mipira hii, bali ikaanze ikatumike kwa maandalizi ya michezo ya Umitashumita na Umiseta.Taifa.
Kipekee amempongeza sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassàn Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maboresho makubwa ambayo ameyafanya katika Sekta ya Michezo Nchini ambuapo sasa kupitia timu zetu tunashuhudia mafanikio mbalimbali.
Halmashauri zilizonufaika na gawiwo hili ni Manispaa ya Kahama wanapewa mipira 200, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga 200, Ushetu 150, Msalala 150, Kishapu 150 na Manispaa ya Shinyanga mipira 150.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa