Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Dibisheni ya Ardhi na Mipango Miji Manispaa ya Kahama ili kupisha uchunguzi kufuatia msululu wa malalamiko dhidi yao huku akiwataka watumishi wote Mkoa wa Shinyanga kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, sheria, utu na bila dhuluma ili wananchi wananchi wafurahie huduma zitolewazo na Serikali.
Tukio hili limetokea leo tarehe 29 Februari, 2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Parking ya Malori uliopo Kata ya Majengo hapa Manispaa ya Kahama wenye leongo la kupokea, kusikiliza na kuzipatia majawabu kero zote za wananchi.
Akizungumza katika hitimisho la mkutano huu RC MNDEME amesema, kumekuwepo na msululu wa malalamiko dhidi ya watumishi wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Kahama, jqmbo linalopelekea kunyooshewa vidole kila kiongozi anapokuja Kahama huku majina yanayotajwa ni yaleyale yanajirudia.
"Kunekuwepo na malalamiko mengi sana Idara ya Ardhi hapa Manispaa ya Kahama, kero hii imekuwa ikiripotiwa kila ugeni wa kiongozi yeyote anayefika hapa na majina yanayotajwa ni hayahaya. Kufuatia msululu wa malalamiko haya, wafuatao watapisha uchunguzi ili watakapobainika hawana hatia watarejeshwa watumishi hawa ni Clemence Mkusa ( Mkuu wa Divisheni ya Ardhi na MipangoMiji ), Yusuph Shaban ( Afisa Ardhi Mteule ), Yahaya Msangi ( Mpima Ardhi ) na Crispine Kisengo ambaye ni Afisa Mipango Miji," amesema RC MNDEME.
Kando na hili RC MNDEME pia ametatua kero ya viwanja 14 mali ya Calorine Magege ya kupatiwa haki yake, mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 6 sasa, huku akimuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kahama kuhakikisha anawafuatilia na kuwakamata wamiliki wa nyumba zinazojihusisha na ukahaba sanjali na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na ukahaba pamoja na wanunuzi wao.
Picha ikimuonesha RC MNDEME (kulia) akiwa na RAS SHINYANGA Prof. Siza Tumbo wakati wa mkutano wa hadhara kusikiliza na kutatua kero za wananchi Manispaa ya Kahama
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa