Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka vijan kuitumia mitandao ya kijamii kujielisha zaidi ili kupata maarifa yatakayo wawezesha kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kujitangaza na kutafuta masoko nje ya eneo lao la kazi.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 20 Julai, 2023 alipotembelea na kuzungumza na Kikundi cha Watengeneza Masofa kilichopo Kalola katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambapo pamoja na maelekezo mengine aliwasifia vijana hao kwa kazi nzuri wanazozifanya huku akiwata kuonesha shukurani zao kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi zaidi baada ya kuwa wamenufaika na mkopo usiokuwa na riba wa Milioni 30.
"Kwanza niwapongeze sana kwa kazi nzuri za ubunifu mnazozifanya haoa katika karakana yenu, lakini niwatake sasa kutumia mitandao ya kijamii kujiongezea maatifa kwa kusoma, kujitangaza ninyi na bidhaa zenu na kutafuta masoko ili muweze kuuza ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga pamoja na nje ya nchi yetu kwakuwa kazi zenu ni nzuri sana," alisema Mhe. Mndeme.
Kando na hayo, pia Mhe. Mndeme akiwata vijana hao kutokubali kudanganywa na baadhi ya watu wanaoeneza maneno yasiyokuwa na ukweli kwamba nchi itauzwa au bandari inauzwa jambo ambalo siyo kweli kabisa, Serikali ipo makini sana na kilichofanika katika suala la Bandari ni mkataba wa makubaliano ya kuboresha utoaji wa huduma.
Kwa upade wake Ndg. Luhanya Anatory Sita ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi kwa niaba ya wenzie alimshukuru sana Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwakopesha Milioni 30 bila riba jambo ambalo limeborsha sana kazi zao. Kisha akamshukuru pia Mhe. Mndeme kwa kuwatembelea katika katakana yao huku wakisema kuwa kitendo hicho kinawapa moyo na imani kubwa sana kwamba Serikali ipo pamoja nao na ndio maana iliwakopesha fedha zisizo na riba ili kuboresha kaai zao.
Awali Mhe. Mndeme akiwa ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Mboni Mhita alitembelea, kukagua na kushiriki kazi mbalimbali za kijamii ambapo alipalili eneo la kupandia miti 500 katika Zahanati ya Kijiji cha Masabi, kuteremsha tofali katika Kituo cha Afya Segese kitakachokuwa kinahudumia vijiji zaidi ya vitano na kukutana na wanafunzi ambapo aliwakumbusha wajibu wao wa kusoma kwa bidii kwani Serikali imekwisha walipia gharama zao zote.
Ziara hii ni hitimisho ya mfululizo wa siku 4 ambapo Mhe. Mndeme ambaye aliongozana na Kamati a Usalama ya Mkoa na ameweza kuzitembelea Halmashauri 6 zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga na kukagua miradi 42 itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2023 ambapo kwa ujumla wake ameridhishwa na maandalizi yote.
Mhe. Mndeme akimsikiliza mwenyekiti wa Kikundi cha Vijana Watengeneza Masofa Ndg. Luhanya Anatory Sita (wa tatu kutoka kulia) akielezea jambo kuhusu kikundi chao
Mhe. Mndeme akionekana kwenye picha wakati akishiriki shughuli mbalimbali za kijamii akiwa na Mkurugenzi wa Msalala Ndg. Khamis Katimba na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa