Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amezindua rasmi uzalishaji wa Almasi katika Mgodi wa Mwadui (Williamson Diamond LTD) na kuagiza kuongezwa kasi ya ufanisi zaidi katika uzalishaji.
Mhe. Mndeme ameyasema leo tarehe 17 katika uzinduzi huo rasmi na kuashiria kuanza rasmi kwa uzalishaji ukiohuduriwa na viogozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, Mbunge wa Jimbo la Kishapu pamoja na wataalamu mbalimbali huku akiutaka uongozi wa Mwadui kuanza mara moja kwa usanifu wa bwawa jingine mbadala wa hili la sasa iwapo litajaa liwepo jingine tayari kwa kuendeleza shughuli badala ya kuwa na bwawa moja na punde inapotokea hitirafu inakuwa ni vigumu kendeleza kazi jambo ambalo linapelekea wao kukosa mapayo, Serikali kukosa mapato, kusimama kwa miradi ya maendeleo na kupunguza uchumi wa kipato kwa wafanyakazi wa mgodi pia.
"Kwanza niwapongeze sana uongozi wa Mgodi wa Mwadui pamoja na watumishi wote kwa kuanza tena kwa kazi za uzalishaji kwa wakati, kwani nilipokuja mimi niliagiza muanze kazi kabla ya tarehe 1 Agosti, 2023 na alipokuja Mhe. Dkt. Dotto Biteko aliagiza kuanza muanze tarehe 15 Julai, 2023 na ninyi mmeanza ndani ya muda mliopewa hongereni sana kwa hili, lakini pia niwatake muanze usanifu wa bwawa mbadala wa hili ili kuwa na tahadhari inapotokea shida liwese kusaidia," alisema Mhe. Mndeme.
Akizungumza wakati wa hitimisho la uzinduzi wa uzalishaji Meneja wa Mgodi Mhandisi Ayoub Mwenda alisema kuwa, wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kwamba bwawa la majitope maji lililopo hivi sasa litadumu kwa muda wa miaka miwili lakini wakati huu likiendelea kuhudumia wataanza usanifu wa bwawa mbadala kama ilivyoshauriwa na Mhe. Mndeme ambalo litakuwa ni muda mrefu zaidi ili kuweza kwenda na kasi pamoja na maelekezo ya Serikali katika kukidhi matarajio ya Mgodi na Serikali pia.
Awali akiongea katika tukio hilo, Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo aliwapongeza sana Mwadui huku akisema kuwa sasa utekelezaji wa miradi ya maedeleo kwa wana Kishapu itarejea kama zamani kwani walikuwa wakinufaika kupitia sehemu ya mrejesho wa faida yao ambayo ilikuwa ikienda kutekeleza miradi yao ya maendeleo.
Mgodi wa Mwadui umeanza tena rasmi uzalishaji baada ya kuwa umesimama kwa takribani miezi nane sasa tangu kutokea kwa hitirafu iliyopelekea kubomoka kwa tuta la majitope jambo ambalo lilipelekea kusitishwa kwa uzalishaji wa Almasi katika eneo hilo.
Picha na matukio wakati wa uzinduzi
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa