Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ambao hawajahamia makao makuu ya Halmashauri hiyo, kata ya Nyamilangano, wahamie mara moja vinginevyo watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Telack ametoa agizo hilo leo tarehe 30/01/2020 katika ziara yake kwenye Halmashauri hiyo, alipokwenda kwa lengo la kukagua usimamizi wa miundombinu ya shule.
Akiwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Mhe. Telack amekagua daftari la mahudhurio na kubaini kuna utoro na uchelewaji mkubwa wa baadhi ya Watumishi kutokana na wengi wao kuishi Kahama mjini.
"Watumishi wote ambao hawajahamia Ushetu nipate orodha yao kwa majina na kuanzia leo naanza kuwachukulia hatua" amesema Mhe. Telack.
Aidha, amewataka Wakuu wa shule zote Mkoani hapa kusimamia ufundishaji na mahudhurio ya wanafunzi ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mitihani ya mwisho.
"Hatutaweza kufanya vizuri kwenye taaluma kama Wakuu wa shule hamsimamii ufundishaji" amesema.
Naye Katibu Tawala Mkoa Bw. Albert Msovela amewataka watumishi wote kusimama kwenye nafasi zao na kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa