Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KAMATI ya Ushauri ya Mkoa wa Shinyanga (RCC) ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa Mhe. Anamringi Macha imejiridhisha na pendekezo la kugawa Jimbo la Uchaguzi la Solwa kuwa Majimbo ya Sllwa na Itwanhi baada ya kukidhi vigezo vya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC) na kwamba Jimbo lina ukubwa wa Kilometa za mraba 4,212 na kiutawala likiwa na Tarafa 3, Kata 26, Vijiji 126 na Vitongoji 856.
Hayo yamejiri wakati wa RCC Maalum ikiyoketi tarehe 15 Machi, 2025 katika Ukumhi wa Mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, ambapo pamoja na mambo mengi RC Macha aliwaeleza wajumbe kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya mchakato huo kupitia hatua zote muhimu ikiwemo kujadiliwa katika Baraza la Waheshimiwa Madiwani na Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Shinyanga (DCC) na sasa RCC.
"Ndugu wajumbe wa RCC tumekutana hapa maalum kujadili pendekezo la kuligaw Jimbo la Uchaguzi la Solwa na kuwa Majimbo mawili yaani Solwa na Itwangi, na hii inakuja baada ya kuwa taratibu zote zimefuatwa na kuzingatiwa ikiwemo kukidhi vigezo vya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania na kujadiliwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Shinyanga na sasa ni zamu yetu RCC," alisema RC Macha.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Jimbo la Solwa lilikuwa na jumla ya wakazi 468,611 ambapo kwa sasa inakadiriwa kuwa na zaidi ya watu 503,167 idadi ambayo ni kubwa sana kwa Mbunge mmoja kuhudumia wananchi kikamilifu.
Kwa taarifa hiyo, Jimbo la Solwa litakuwa na Tarafa moja (01) ya Nindo yenye jumla ya Kata 12 ambazo ni Salawe, Mwenge, Solwa, Mwakitolyo, Lyabukande, Lyamidati, Iselamagazi, Lyabusalu, Pandagichiza, Mwalukwa, Mwantini na Nyamalogoa. Jimbo litakuwa na Vijiji 68 na Vitongoji 478.
Jimbo la Itwangi litakuwa na Tarafa mbili (02) ya Itwangi na Samuye zenye jumla ya Kata 14 ambazo ni Ilola, Didia, Puni, Itwangi, Nyida, Tinde, Nsalala, Usule, Bukene, Imesela, Mwamala, Samuye, Masengwa na Usanda. Jimbo litakuwa na jumla ya Vijiji 58 na Vitongoji 378.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa