Na. Paul Kasembo. RS SHY.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 21 Mei, 2024 amekutana na Uongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Mhandisi Julieth Payovela akiwa na Mkurugenzi wa LifeWater International Nchini Tanzania Ndg. Devocatus Kamara pamoja na sehemu ya watumishi wenzao kwa lengo la kujitambulisha na kueleza shughuli za maendeleo wanazozifanya Mkoani Shinyanga.
RC Macha amemshukuru sana mdau huyu wa maendeleo ambaye amekuwa akitekeleza miradi mikubwa na yenye tija kwa wananchi pamoja na Serikali kwa lengo la kuboresha na kusogeza karibu huduma kwa wananchi wa Shinyanga.
Aidha wameweza kujadili na kuwekeana mikakati wa kukamilisha mradi wa Mwalukwa wenye thamani ya zaidi ya Bil. 1.05 ili uweze kuendelea kuwanufaisha wananchi wa Kata hiyo na maeneo jirani.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa