Na. Shinyanga RS
MKUU wa mkoa wa shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini kazi zote zinazofanywa na Walinzi wa Jadi (sungusungu) katika maeneo yao huku akiwataka kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote za nchi ili kuepusha hali ya sintofahamu kutoka kwao kwani wao wanamchango mkubwa sana katika kulinda amani ya nchi yetu.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 18 Oktoba, 2023 alipokuwa akizungumza katika sanjo iliyojumuisha machifu, watemi, viongozi na sungusungu wa mikoa mitano ya Mwanza, Simiyu, Geita, Tabora na wenyeji Shinyanga kwa lengo la kufahamiana, kuhuisha majukumu yao ya kila siku, kusikiliza na kutatua kero zao hafla iliyojumuisha pia viongozi wa serikali zikiwemo Kamati ya Usalama, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo, mkuu wa wilaya Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita, mbunge wa Jimbo la Kahama Mhe. Jumanne Kishimba na wengine wengi.
"Ndugu zangu wanausalama Walinzi wa Jadi maarufu sungusungu wa sanjo hii ya mikoa mitano ya mwanza, simiyu, geita, tabora na mkoa wetu wa shinyanga ambao ndiyo wenyeji wa sanjo hii, nipende kuwaeleza kuwa serikali inatambua na kuthamini sana kazi zenu hizi kwa jamii. Lakini nawataka nanyi kwenda kufanya kazi zenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi ioi kuendeleq kuaminika kwa umma ambao umnqutumikia" alisema Mhe. Mndeme.
Sajali na hayo, Mhe. Mndeme pia amewaagiza viongozi wote mkoa wa shinyanga kuhakikisha wanawapatia ushirikiano wa kutosha sungusungu hao kwani wanamchango mkubwa sana katika kulinda amani, kukuza uchumi na kutumikia taifa letu kwa ujumla huku akiwqkumbusha wajibu wa kupanda miti na kutunza mazingira pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwetu.
Awali akitoa salamu za kitaifa Mshauri wa Sungusungu Taifa ndg. Idi Ame pamoja na kuwapongeza lakini alishauri walinzi wa jadi kuwa na sare ya nguo zao pamoja na fimbo zao pia ioi kuondoa sintofahamu ya mavazi yao kamq yalivyo sasa hivi.
Kwa upande wake Mhe. Kishimba alishauri sungusungu kuwa na mfuko wa kusaidizana kwenye shida na raha, kuwepo na bima afya kwa familia zao.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa