• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI YAPOKEA TAARIFA YA UCHUNGUZI MIGODI YA WACHIMBAJI WADOGO MWAKITOLYO - SHINYANGA

Posted on: November 11th, 2023

Na. Shinyanga RS.

WAZIRI wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (MB) leo akiwa katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga amepokea taarifa uchunguzi migodi ya wachimbaji wadogo Mwakitolyo yaliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Shinaynga huku akiwahakikishia kuwa hakuna mchimbaji yoyote atakayeondelewa katika eneo hilo.

Katika taarifa iliyofanywa na timu ya wataalamu kuhusu uchambuzi wa mikataba kati ya Vikundi vya wachimbaji wadogo wa madini na mwekezaji kwenye leseni za uchimbaji mdogo zilizopo katika eneo la Mwakitolyo mkoani Shinyanga kamati imebaini sehemu kubwa ya maduara hayapo katika hali salama  ya uchimbaji.

Taarifa hiyo imebainishwa leo oktoba 11,2023 na  mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi kutoka Wizara ya Madini Mhandisi Ally Samaje wakati akiwasilisha taarifa ya uchunguzi kwa Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde mkoani Shinyanga.

Mhandisi Samaje amesema kuwa katika kipindi cha kati ya mwezi Septemba 2022 hadi Oktoba 2023, mitambo 137 ya kuchenjulia dhahabu katika eneo la Mwakitolyo imezalisha takribani kilogramu 1,162 sawa na tani 1.162 , kati ya kiasi hicho kilogramu 639ambazo sawa na asilimia 55 imetoka katika eneo la Nyaligongo.

Akielezea kuhusu utaratibu wa kuingiza na kutoa malighafi zinazotokana na u chimbaji madini katika eneo la Mwakitolyo Mha.Samaje amesema idadi ya  vibali 1578 vya uchimbaji madini vitolewa na kuzalisha tani 271,278 za mbale kutoka eneo la Nyaligongo.

Aidha , Mhandisi Samaje ameshauri kuwa Mkaguzi wa Migodi asimamie mpango maalumu wa uchimbaji madini kwa kufanya ukaguzi mara kwa mara pamoja na kuwashauri namna bora ya kuendesha shighuli za uchimbaji kwa usalama.

Kwa ujumla kamati ilibaini yafuatayo,


● Kamati yabaini maduara

hai 65 kati ya maduara 1297,


● *Ni maduara 6 tu yenye Uzalishaji kati ya maduara 134,


● Septemba 2022 hadi Oktoba 2023 tkribani kilogramu 1,162 za dhahabu zimetoka Mwakitolyo,


"VISION 2030" MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI.

Eng. Ally Samaje Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguziWaziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde (MB) akiwa na Prof. Siza Tumbo (kushoto) ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga wakati wa mkutano wa wachimbaji wadogo katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa