Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaambia wanunuzi na wakulima wa zao la Pamba kuwa Serikali ipo kuhakikisha wote wananufaika na uuzaji wa zao hilo wakati wa ziara yake mapema jana tarehe 09/08/2019 Mkoani Shinyanga.
“Nataka niwahikikishie Serikali imejikita kuhakikisha ubora kuanzia kwenye maandalizi, kilimo chake, pembejeo na kuhakikisha masoko anapatikana”
Amesema kutokana na zao la Pamba kuuzwa Kimataifa, hivyo hali ya soko la nje kuwa bei ndogo na soko la ndani limeyumba pia, kwa hali hiyo Serikali pamoja na wanunuzi wamekaa na kutafakari namna gani ya kuiondoa pamba kwa wakulima.
Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa rai kwa wanunuzi wenye viwanda vya kuchambua pamba kujitanua zaidi kufikia viwanda vya kutengeneza nguo na kuwa, Serikali itawaunga mkono kwa kila hatua.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa