Mwanariadha wa Shinyanga Makoye Bundala ameibuka kuwa mshindi wa kwanza katika fainali za mbio za mita 100 za mashindano ya UMITASHUMTA zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Makoye ametumia muda wa sekunde 11:87, ambapo aliyemfuatia ni Matiko Nyamalaga kutoka mkoani Mara ambaye alitumia muda wa sekunde 11:94, na nafasi ya tatu imechukuliwa na mwanariadha Steven Stephano wa Tabora ambaye aliyetumia muda wa sekunde 12:07 kumaliza mbio hizo.
Kwa wasichana, mshindi wa fainali za mbio za mita 100 ni Shija Donald wa Mwanza ambaye ametumia muda wa sekunde 13:16 kumaliza mbio hizo, nafasi ya pili imechukuliwa na Paulina Pius pia wa Mwanza ambaye ametumia muda wa sekunde 13:38, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Fauzia Hamu wa Singida ambaye ametumia muda wa sekunde 13:91.
Katika mchezo wa kurusha mkuki nafasi ya kwanza imechukuliwa na mwanafunzi Suzan
PICHANI: Mwanariadha Makoye Bundala (501) wa Shinyanga akimaliza mbio za mita 100 wavulana mbele ya Matiko Nyamalaga (289) wa Mara na Steven Stephano wa Tabora (601).
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa