• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

SHIRECU, HAKIKISHENI MNAJISAJILI KIDIGITALI ILI MUENDESHE CHAMA KIBIASHARA ZAIDI - KAKOZI IBRAHIM

Posted on: March 28th, 2025

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

Mrajisi Msaidizi wa Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Ndg. Kakozi Ibrahim amekitaka Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) 1984 LTD kuweka kipaumbele na kuhakikisha wanajisajili na kutumia mifumo ya kidigitali ili kuendesha Chama kibiashara zaidi pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali katika shughuli za uzalishaji na biashara kwa maslani mapana ya Chama.

Ameyasema haya Machi 28, 2025 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 30 wa SHIRECU uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa SHIRECU uliopo Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na yote ameongeza kuwa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) inasisitiza Vyama vya Ushirika kuwa na akaunti za Benki katika Benki ya Maendeleo ya Ushirika ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya mifumo ya kidigitali katika uboreshaji wa vyama.

“Pamoja na kuwapongeza kwa jitihada mnazofanya lakini ninawasisitiza kuweka kipaumbele cha kuhakikisha mnajisajili na kutumia mifumo ya kidigitali ili kuendesha chama kidigitali na kibiashara zaidi sambamba na kushirikiana pamoja na wadau mbalimbali katika shughuli za uzalishaji na biashara kwa maslahi ya kufanya chama kisonge mbele zaidi,” amesema Ndg. Ibrahim.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa SHIRECU Bi. Asnath Changamike akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji ya Bodi amesema kuwa kuanzia Aprili 2024 hadi kufikia Machi 2025 chama kimefanikiwa kukusanya takribani Tzs. Bilioni 1 ambayo ni sawa na asilimia 68.61 ya ukusanyaji wa mapato kupitia shughuli za ndani za chama.

Aidha ameongeza kuwa SHIRECU imefanikiwa pia kusajili Vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) takribani 127 pamoja na kusajili wanachama wapatao elfu 30 kwenye Mfumo wa Kielekroniki wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) ili kuwaunganisha ili kuwa na ukaribu kupitia mifumo hiyo ya kidigitali.

Mkutano Mkuu wa 30 wa SHIRECU 1984 LTD pamoja na mambo mengine umejadili, kupokea na kuhuisha sera mbalimbali za Ushirika, kujadili na kupitisha ukomo wa madeni sambamba na kupokea taarifa ya utekelezaji ya Bodi na kupitisha bajeti ya chama kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MRADI WA TABLET KWA SHULE ZA MSINGI WATAMBULISHWA NGAZI YA MKOA WA SHINYANGA NA WILAYA

    June 03, 2025
  • SHINYANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA REA, WAUZIWA KWA RUZUKU MITUNGI 13000

    June 02, 2025
  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa