Sabasaba, Dar es Salaam.
Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza rasmi kwa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba mwaka 2025, wananchi pamoja na wageni kutoka maeneo mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi kutembelea, kununua bidhaa na kupata huduma mbalimbali katika mabanda ya Mkoa wa Shinyanga.
Hali hii imekuwa chachu ya mafanikio kwa wafanyabiashara wetu kwa kuwawezesha kupata fursa ya ya kukutana, kubadilishana uzoefu, na kujifunza kutoka kwa wenzao kutoka mikoa na mataifa mbalimbali.
Ushiriki wa Mkoa wa Shinyanga kupitia uratibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa unaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuwatangaza Wafanyabiashara wa ndani ya Mkoa, kutangaza bidhaa na hudjma zao, kutangaza fursa zilizopo mkoani, katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, uwekezaji, viwanda, miundombinu, kilimo, mifugo, afya, uongezaji thamani bidhaa, maji nk. Fursa hizi zimekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi.
Kupitia maonesho haya, uongozi wa Mkoa unaendelea kujenga uwezo na kujiamini katika kushawishi na kuvutia wawekezaji zaidi kuja kuwekeza Shinyanga. Hili linawezekana kutokana na mazingira rafiki na wezeshi yanayoendelea kuimarishwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Serikali imeendelea kuweka mazingira bora kwa ajili ya uwekezaji, yakiwanufaisha wawekezaji wazawa na wageni kwa pamoja.
Mkoa wa Shinyanga unawakaribisha wadau wote kutembelea mabanda yetu ili kujionea fursa zilizopo na kushirikiana nasi katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa