Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Ndg. Donasian N. Kessy amesema kuwa Taasisi yake imejipanga kufanya warsha na kusimamia utekelezaji wa maazimio yote ya changamoto mbalimbali zilizobainika kwenye chambuzi za migumo na miradi ya maendeleo.
Haya yamesemwa leo tarehe 23 Aprili, 2024 na Ndg. Kessy katika mkutano na wanahabari alipokuwa akitoa Taarifa kwa Umma kwa kipindi cha robo ya tatu Januari - Machi, 2024 ambapo amesema kuwa TAKUKURU Shinyanga kwa kipindi cha Aprili - Juni, 2024 itajielekeza zaidi kwenye ufuatilia wa fedha za miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa thamani halisi ya fedha kama Serikali ilivyokusudia.
" Pamoja na mambo mengine, Taasisi ya TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga tumejipanda kufanya warsha na kusimamia utekelezaji wa maazimio yote ya changamoto mbalimbali zilizobainika kwenye chambuzi za mifumo na miradi ya maendeleo," amesema Ndg. Kessy.
Ndg. Kessy pia ameongeza kaa kusema kuwa ofisi imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa Elimu ya masuala ya rushwa yanatolewa katika Taasisi za Serikali, binafsi na wananchi ili kuongeza wigo wa mapambano dhidi ya rushwa.
Kwa ujumla TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali na kazi hizo ni kama vile; Uimarishaji wa klabu za wapinga rushwa 35, mikutano ya hadhara 17, semina 11, vipindi vya redio 4, na maonesho matano (5).
Mwisho TAKIKURU imetoa wito kwa wananchi wote Mkoani Shinyanga kutoa ushirikiano kwa Serikali, kuhakikisha miradi yote inayoendelea inakamilika kwa ubora uliokusudiwa.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa