TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imesema kuwa imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya SEQUIP Mkoani hapa ambapo kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo TAKUKURU ilifanya ufuatiliaji katika miradi ya Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari SEQUIP ili kuona kama miradi hii inatekelezwa kwa wakati na katika ubora wa viwango vinavyohitajika.
Hayo yamesemwa leo tarehe 7 Februari, 2024 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Ndg. Donasian Kessy alipokuwa akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari ofisini kwake ambapo pamoja na mambo mengine pia amesisitiza umuhimu wa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutoa ushirikiano kwa serilkali ili kuhakikisha miradi yote inayoendelea katika Mkoa wetu inakamilika kwa wakati na kwa ubora.
"TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga umeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Mpango wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari SEQUIP, na hivyo basi natoa wito kwa wananchi Mkoa wetu kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kuhakikisha kuwa miradi hii inakamilika kwa wakati na kwa ubora stahiki," amesema Kessy.
Aidha, TAKUKURU imejiwekea mikakati ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2024 ambapo itajikita zaidi kwenye ufuatiliaji wa fedha za miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa thamani halisi ya fedha kama serikali ilivyokusudia. Pia itaendelea kufanya warsha za kusimamia utekelezaji wa maazimio yote ya changamoto mbalimbali zilizobainika kwenye chambuzi za mifumo na miradi ya maendeleo.
KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU; TUTIMIZE WAJIBU WETU
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Ndg. Donasian Kessy akielezea jambo wakati akizungumza na wanahabari (hawapo hewani)
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa