Na. Paul Kasembo, SHY RS
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amesema kuwa Tanzania imeendelea kupiga hatua kubwa kimaendeleo katika Sekta mbalimbali nchini tangu tupate uhuru mwaka 1961 kwani mpaka sasa uwekezaji unazidi kuongezeka na hivyo kutokeza fursa kwa wananchi hususani vijana kujiingizia kipato na kukuza uchumi wa Taifa.
Wakili Mtatiro ameyasema haya leo tarehe 9 Desemba, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, maadhimisho ambayo kimkoa yamefanyika katika Shule ya Msingi Mhangu iliyopo Kata ya Salawe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
“Tangu Tanzania tupate uhuru mwaka 1963, tumeendelea kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika Sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, elimu, afya, maji, miundombinu nk. kwani mpaka sasa uwekezaji unazidi kuongezeka na hivyo kutokeza fursa nyingi kwa vijana kujiingizia kipato na hatimaye kuchangia kukuza uchumi wa Taifa letu” amesema Mtatiro.
Aidha ameongeza kwa kuwasisitiza wananchi mkoani Shinyanga kushiriki katika zoezi la upandaji miti katika maeneo wanayokaa kwa kushirikiana na viongozi wa Vijiji na Vitongoji ili kuifanya Shinyanga iwe ya kijani na ya kuvutia zaidi.
Maadhimisho haya kwa Mkoa wa Shinyanga yameambatana na shughuli mbalimbali za kijamii zikiwemo upandaji miti, upimaji afya na burudani mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuenzi na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa Wanashinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa