UONGOZI WA UFUNGAJI MRADI MGODI WA BUZWAGI WAJITAMBULISHA.
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na kuzungumza na sehemu ya uongozi wa Mradi wa Ufungaji Mgodi wa Buzwagi ukiongozwa na Zonnastral Mumbi ambaye ni Meneja Ufungaji Mgodi na Stanley Joseph ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Jamii na Miradi waliofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha sanjari na kuelezea mikakati endelevu kuelekea ufungaji mradi huu wa Buzwagi uliopo ni Kahama.
Pamoja na mambo mengine, RC Macha amewapongeza sana Menejimenti ya Buzwagi kwa namna ambavyo utekelezaji wa ufungaji mradi huu unavyotekelezwa huku akiwaahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi na kwamba itafanya kila liwezekanalo katika kuwawekea mazingira kuwa rafiki na wezeshi wakezaji wote katika Mkoa wa Shinyanga wakiwemo na Buzwagi Gold Mining.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa