Na. Paul Kasembo, Shinyaga DC.
MWEZESHAJI kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ndg. Datius Rwebigene amewakumbusha viongozi waliochaguliwa katika ngazi ya Vijiji na Vitongoji kwamba, pamoja na majukumu mengine lakini ni muhumi sana kuhakikisha wanakwenda kusoma mapato na matumizi katika vikao na mikutano yao watakayoifanya kwenye maeneo yao.
Datius aliwakumbusha hayo wakati wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wenyeviti takribani 982 wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Shinyanga ambapo pia wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu, uzalendo, kudumisha amani, kufanya kazi kwa kuzingati sheria, kanuni na taratibu za nchi na kusimamia vyanzo vya mapato.
Mafunzo ya kuwajengea uwezo wenyeviti yanafanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekwzo ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha aliyeelekeza kupewa mafunzo na kuwajengea uwezo viongozi wote waliochaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa