Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba amesema watoto wa kike wakilindwa na kuendelezwa ni chachu ya kufikia maendeleo ya uchumi wa kati ikiwa ni lengo la Serikali ya Awamu ya tano.
Akizungumza na watendaji na wadau wa masuala ya kuwalinda watoto, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 03/06/2019 wakati wa kikao cha kufunga miradi miwili ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na vijana, iliyotekelezwa na shirika la "Save the Children kwa miaka miwili Mkoani hapa.
"Hakuna Taifa lililoendelea kama wanawake wapo nyuma" amesema Mhe. Taraba na kuwataka wadau wote kuhakikisha watoto wa kiume na wa kike wana haki ya kuendelezwa na kulelewa sawa.
Taraba amesema kuwa, watoto sasa hivi wameachwa wanajilea wenyewe tofauti na zamani, wazazi wamekuwa mbali na wanashindwa kuongea na watoto wao hivyo kuchangia watoto na vijana wengi kushawishika kufanya matendo maovu ikiwemo ngono na hatimaye kutotimiza ndoto zao.
Amewaomba wadau kuendelea kushirikiana na Serikali kuwalinda watoto hawa, kwani bado kuna changamoto kubwa katika Mkoa wa Shinyanga hasa suala la mimba za utotoni.
Shirika la Save the Children limehitimisha utekelezaji wa miradi yake miwili, Mradi wa Ulinzi wa Mtoto na usimamizi wa utekelezaji wa Haki za Mtoto, pamoja na mradi wa kutokomeza Mila na Desturi kandamizi kijinsia ambayo imeweza kuwafikia watoto na vijana katika Halmashauri tano na vijiji 150 Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu akizungumza na wadau wa watoto wakati wa kufunga mradi wa kulinda haki ya mtoto na vijana
Bw. Jesse Munegezi, Mkurugenzi Msaidizi uendeshaji wa Shirika la Save the Children, akitoa taarifa ya miradi ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na vijana
Washiriki wa kikao cha kufunga miradi miwili ya kuwalinda watoto na vijana wakimsikiliza Mgeni rasmi Mhe. Nyabaganga Taraba
Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia kwa makini mada ya video ya jinsi miradi hiyo ilivyotekelezwa
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa