Kituo cha Afya cha kata ya Songwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kinatarajiwa kukamilika baada ya wiki mbili ambapo kitahudumia wananchi 21,500 wa kata hiyo na vijiji jirani.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu ndg. Charles Kabeho, mtendaji wa kata hiyo Bi. Annastazia Machanya amesema kuwa, Kituo hicho kilichogharimu jumla ya sh. Milioni 400 kimejengwa kupitia fedha za mpango wa kuimarisha huduma za afya kutoka Serikali kuu.
Akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho, ndg. Kabeho ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha za kuimarisha vituo vya Afya na wasimamizi wa mradi huo uliojengwa kwa viwango.
Mwenge wa Uhuru umeingia Mkoani Shinyanga ukitokea katika Mkoa wa Simiyu mapema tarehe 20/08/2018 ambapo utakimbizwa katika Halmashauri zote sita na kupitia miradi ya maendeleo 49 yenye jumla ya sh. bilioni 28.3 ikiwa ni michango kutoka Serikali kuu, Halmashauri, Wananchi na Wahisani.
Katika siku ya kwanza Wilayani Kishapu, Mwenge wa Uhuru umepitia miradi 10 ya maendeleo yenye gharama ya sh. Bil.2.2.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa