Na. Paul Kasembo, SHY RS.
Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) Dkt. Beatrice Mwalike amesema kuwa wakunga ni nguzo muhimu katika huduma za afya ya uzazi, na kuwa wao ni sehemu ya mchakato wa kupunguza vifo vya mama na mtoto huku akitoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga kuyatumia maadhimisho hayo kwenda kupata huduma mbalimbali eneo hilo ambapo kilele chake ni Mei 5, 2025.
Dkt. Mwilike alisema hayo Mei 4, 2025 wakati wa mkutano na wandishi wa habari uliofanyika katika viwanja vya Zimamoto Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiho kutoa wiyo kwa Serikali, UNFPA na Wadau wa afya kuendelea kuwekeza kwa wakunga kwa kuwapa mafunzo, vifaa na mazingira boranya kufanyia kazi.
"Wakunga ni nguzo muhimu katika huduma za afya ya uzazi, hasa wakati wa migogoro, majanga ya asili, na mabadiliko ya tabia ya nchi, huduma zao haziwezi kuahirishwa na wanahitaji msaada wa kutosha ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wetu, alisema Dkt. Beqtrice.
Inatajwa kwamba, kwa kuwapa wakunga msaada unaohitajika, Tanzania inaweza kufikia malengo ya kuhakikisha kila mama anajifungua kwa usalama hata wakati wa migogoro na majanga Wakunga wanaweza kuchangia kwa asilimia 90 ya kupunguza vifo vya mama na mtoto, kwa hiyo, uwekezaji kwa wakunga ni uwekezaji kwa maisha ya mama na mtoto.
TAMA pia inatangaza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika mkoani Shinyanga, katika viwanja vya Zimamoto kuanzia Mei 4- 5 Mei, 2025 ambapo huduma za afya bure zitapatikana kwa wananchi sanjari na mabanda ya maonyesho ya kazi mbalimbali za wakunga yakionyesha mchango wao katika jamii.
Mei 5, 2025 ni kilele ambapo kutatanguliwa na matembezi ya wakunga kuonyesha kazi zao na kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa huduma za uzazi.
Kauli mbiu ni "Mkunga ni Nguzo Muhimu katika kila Janga".
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa