#shinyanga_rs
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndugile amewasisitiza wamiliki na walezi wa makao ya watoto yatima wanaoishi katika mazingira hatarishi kwenye Halmashauri ya Kishapu, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Shinyanga kuzingatia taratibu zote za uendeshaji wa makao, kutoa lishe bora na elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa MPOX pamoja na Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi na Makuzi ya Awali ya Mtoto ili kuboresha utoaji wa huduma.
Dkt. Yudas ameyabainisha haya Machi 14, 2025 wakati akifungua kikao cha kuwajengea uwezo wamiliki na walezi wa makao ya watoto yatima mkoani Shinyanga ambapo pia amewaasa kuboresha mawasiliano na kuwa na umoja wa wamiliki wa makao ili kuwezesha utoaji bora wa huduma kwa watoto.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa