Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MWAKILISHI wa Katibu Tawala Msaidizi Afya, Lishe na Ustawi Mkoa wa Shinyanga Mjiolojia Faustine Mulyutu amewaasa Wanabari kuwa mstari wa mbele katika zoezi la kutangaza, kuhamasisha na kuihabarisha kikamilifu jamii kuhusu umuhimu wa kushiriki katika zoezi la ugawaji wa vyandarua bila malipo linalotarajiwa kuanza hivi karibuni likiwa na lengo kuu la kupunguza na kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani Shinyanga.
Ameyasema haya leo tarehe 6 Januari, 2025 katika mafunzo ya Uhamasishaji Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua kwenye Kaya bila malipo kampeni ambayo inatarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri zote 6 za Mkoa wa Shinyanga huku ikitajwa kuwa zaidi ya vyandarua 1500 vyenye dawa vitawafikia wananchi lengwa.
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa kusaidia Mapambano dhidi ya Virusi vya HIV, Kifua Kikuu au TB na Malaria (Global Fund) wanafadhiri zoezi hili la ugawaji bila malipo wa ugawaji wa vyandarua bure kwa wananchi kazi ambayo itasimamiwa na Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD) ambapo Tanzania inatarajia kutokuwa na Malaria ifikapo mwaka 2030.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa