Na. Paul Kasembo - Kahama MC
WAKAZI wa Kata ya Mhungula iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama sasa wanaelekea kuondokana na kero ya kukosa hudu a ya maji baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita kumpigia simu moja kwa moja Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso wakati mkutano wa hadhara ukiendelea.
Haya yanetokea katika mkutano wa hadhara ambao alikuwa akiufanya Mhe. Mboni wa kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi moja kwa moja kutoka katika maeneo yao wanayoishi, ambapo hoja ya kutokuwepo kwa maji iliibuliwa na ndipo Mhe. Mnoni akampigia simu Mhe. Aweso ambaye alizungumza nao wananchi kupitia kipqza sauti kilichokuwa kikinasa sauti kupitia simu na kuwaahidi kuwafikishia huduma hiyo.
Kupitia mkutano huo, Mhe. Aweso alimuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira kuandaa na kupeleka makadirio ya bajeti ili Wizara ilete fedha hizo na ziweze kuwafikishia huduma wananchi hao.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mboni ameiagiza KUWASA kuhakikisha inapeleka maji katika eneo la Shule mpya ya Sekondari Nyahanga kabla ya Juni, 30 mwaka 2024
Aidha, kutokana na wananchi kutumia muda mrefu kufuata huduma za Afya, Mhe. Mboni amemuagiza Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kahama kusogeza huduma (Outreach) za kliniki kwa watoto wadogo katika Kata hii ya Mhunhula, ambapo mmiliki wa Shule ya Believe Excellence ameombwa moja ya chumba kwenye jengo lake litumike kwa utoaji huduma hiyo ambapo mmiliki huyu amekubali kutoa darasa kwa ajili ya matumizi hayo.wa wananchi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa