Paul Kasembo, SHY RS.
KAMISHNA wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Leo Komba amewaomba wananchi na wadau wote wa kodi Mkoani Shinyanga kulipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka riba ya 5% itokanayo na adhabu na badala yake wakilipa italeta maendeleo ya Taifa na ufanisi wa kazi za Wizara kwa ujumla huku akisisitiza kuwa mwananchi akilipa kwa wakati hakutakuwq na malimikizo jambo ambalo linapelekea mwananchi kuona kama kodi ni kubwa.
Ameyasema haya leo Februari 12, 2025 kwenye Kikao na Wadau wa Kodi Mkoa wa Shinyanga kilicholenga kupokea, kujadili chanagmoto wanazokabiliana nazo, kuzifahamu na hatimae kuweka makubaliano ili hatimae kulipwa kwa madeni hayo ambayo yanatajwa kuwa ni muda mrefu sasa .
“Wananchi, niwaombe sasa muwe na utamaduni wa kuhakikisha kwamba mnalipa kodi ya pango la ardhi kila mwaka na kwa wakati ili kuepuka riba itokanayo na kuchelewa jambo ambalo kwa sehemu kubwa mnalalamika kuwa ni kubwa, lakini kumbe mngelipia kwa wakati hayo yote yasingekuwepo, na kwa kufanya hivyo kunawezesha Taifa kuimarisha na kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi," amesema Leo Komba.
Aidha amewataka wadau kuwa na kawaida ya kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Ardhi pale wanaposhindwa kuendeleza matumizi ya ardhi wanayomiliki ili Mamlaka husika iwapatie wadau wengine waiendeleze na kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.
Kwa upande wake Afisa Ardhi Mwandamizi Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Halima Nassor amewasihi wananchi kuweka kipaumbele na utamaduni wa kulipa kodi kwa wakati kwani Serikali imeanza utekelezaji wa kutoa Hati Madai za siku 14 kwa watu wote wenye malimbikizo ya kodi ili wajadiliane na kukubaliana kulipa kabla ya kuanza kuchukua hatua za kisheria.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi ndugu Leo Komba, Mkoa wa Shinyanga unadai wadau wake zaidi ya Tzs. Bilioni 3.5 huku akitoa wito kwa wananchi ambao bado wanadaiwa kutumia muda huu wa siku 14 ambazo zimetajwa kuwa ni kipindi cha njia shirikishi ambapo mdeni atapata nafasi ya kwenda ofisi za ardhi na kulipa au kukubaliana namna ya kulipa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa