Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa wito kwa wananchi wote kujitahidi kuitunza amani na utulivu wa nchi yetu ili kuendelea kuwaenzi Mashujaa wetu kwani ikipotea huwa ni vigumu sana kuirejesha, na hata ikirejea haiwezi kuwa kama ilivyokuwa awali huku akiwasisitiza kutenda yaliyomazuri zaidi ili tutakapoondoka tuendelee kukumbukwa kama Mashujaa ambao leo ni maadhimisho yao.
RC Macha ametoa wito huu leo tarehe 25 Julai, 2024 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika Viwanja vya Mashujaa (Mazingira Center) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyombo vya Usalama, viongozi wa dini, wananchi na watu,ishi wa Serikali.
"Nitoe wito wangu kwenu wananchi wote, tujitahidi sana kuendelea kuitunza amani yetu na kuenzi utulivu wa nchi yetu ili isipotee na kutoweka kwa namna yoyote ile, kwani ikiwa hivyo ni vigumu sana kuirejesha na hata ikirejea haiwezi kuwa kama ilivyokuwa awali," amesema RC Macha.
Aidha RC Macha amesema kuwa, waweza kuwa na mali nyingi sana lakini unapokosa amani na utulivu ni sawa na mateso wakati wote kwani huwezi kufurahia chochote kile huku akiwataka wananchi kutosubiria mtu aondoke ndiyo wampongeze, badala yake wampongeze akiwa hai kwani kuna mifano mingi ya mashujaa wa sasa hivi na mfano mzuri ni Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ametenda mengi mema kwa ajili ya wanashinyanga na watanzania kwa ujumla wakena hivyo tunapaswa kumpongeza, kumtia moyo na kumuombea sana ili aendelee kuwatumia vema wananchi wote.
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Tanzania huadhimishwa kila ifikapo tarehe 25 Julai, 2024 ikiwa ni sehemu ya kuwaenzi wale wote waliopoteza maisha yao kwa ajili ya kulipigania na kuhakikisha kunakuwa na amani na utulivu ndani ya Taifa letu.
@shinyangamanispaa @kahamamc_official @shinyangadc_official @kishapudc @msalaladc2023 @ushetudc @shinyanga_tanzania
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa