Na. Paul Kasembo, USHETU
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka wananchi wa Ushetu kutokuwa sehemu ya upotevu wa mali za mkandarasi, na badala yake kuwa walinzi wa vifaa hivyo pindi miradi hiyo inapotekelezwa na watakapoona kuna hata viashiria vya uwepo wa hujuma hizo watoe taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama haraka..
Mhe. Macha ameyasema haya wakati wa hafla ya kuwakabidhi Wakandarasi wazawa kutoka Kampuni ya Salum Motors na Jonta Investment kwa Wananchi watakaoanza ujenzi wa madaraja makubwa manne ya Ubagwe, Kasenga, Ng’hwande na Mwabomba yaliyoathiriwa na mvua za El Nino katika Halmashauri ya Ushetu yatakayogharimu zaidi ya Bilioni 18.05.za Kitanzania.
Hafla ya kuwakabidhi Wakandarasi imefanyika Novemba 30, 2024 katika Kijiji cha Bugomba A, Kata ya Ulewe katika Halmashauri ya Wilaya ya ushetu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (MB) ambaye amekuwa mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni.
Viongozi wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Mabala Mlolwa, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani na wananchi.
Kukamilika kwa ujenzi huu wa madaraja manne kunatajwa kuondoa changamoto na adha ya wananchi waliyokuwa wakiipata ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara msimu wa mvua.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa