Repost #Fred Kibano - Shinyanga
Katibu Tawala Msaidizi (ELIMU) Bw. Samson Hango aliyefungu Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Walimu Kazini (MEWAKA) na kuwataka washiriki wapatao 895 kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili kuinua kiwango cha taaluma shuleni.
Bw. Hango ameyasema hayo tarehe 16 Januari, 2025 Manispaa ya Shinyanga na kuwataka washiriki hao kwenda kutumia ujuzi watakaoupata ngazi ya shuleni kwani Serikali inatarajia matokeo chanya baada ya mafunzo.
Aidha, alisema Mradi wa SEQUIP unatekeleza afua zake ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu na uimarishaji wa ufundishaji na ufundishwaji shuleni, kutoa mafunzo kazini (MEWAKA) hatua ambayo ilichukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza na ujenzi wa miundombinu ya shule za wasishana za Mikoa pia ujenzi wa shule za sekondari za kawaida, shule za sekondari za amali na shule salama ili kuboresha elimu nchini.
Naye Bw. Ladslaus Balige Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendesha mafunzo ya walimu wa sayansi waliopo kazini ambapo jumla ya walimu wa sayansi 881na Wathibiti Ubora wa Elimu 14 wanapatiwa mafunzo hayo.
Aidha, Bw. Balige amesema matarajio ya Serikali baada ya mafunzo hayo kuwa kutakuwa na ongezeko la umahiri wa walimu katika masomo ya sayansi na hisabati kama vile ufundishaji wa mada ngumu na kuongezeka kwa wanafunzi katika elimu ya sekondari ya juu, vyuo vya kati na elimu ya juu katika masomo yanayoambatana na sayansi na hisabati.
Kwa upande wake Dkt. Absalom Mbilingi ambaye ni Mwenyekiti wa wawezeshaji wa Mafunzo hayo (MEWAKA) amewataka walimu kushiriki kikamilifu wakati wote wa mafunzo ili kwenda kuboresha mchakato wa ujifunzaji na ufundishaji nje na ndani ya darasa na pia kwenda kuwawezesha walimu wenzao ngazi ya shule hususani juu ya upimaji wa wanafunzi, ufaraguaji wa zana na njia shirikishi za ufundishaji.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa