Wenyeji wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ni wa Makabila ya Wasukuma, Wasumbwa na Wanyamwezi. makabila mengine ni kama Waha, Wahangaza na WanyamwezI
MAHALI ILIPO
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ni Halmashauri iliyoanzishwa tarehe 23/11/2012 kupitia tangazo la serikali GN 362/2012 kufuatia uamuzi wa serikali wa kuleta huduma karibu wananchi. Hii ni kutokana na kugawanyika kwa Halmashauri ya wilaya ya Kahama katika Halmashauri 3 ambazo ni Halmashauri ya mji wa kahama, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu na Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Halmashauri ipo kaskazini magharibi (kusini mwa ziwa Victoria). Halmashauri ipo kati ya nyuzi za Latitudi 3015° na 4030° kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitudi 31030° na 33000° kusini mwa mstari wa Griniwichi. Halmashauri imepakana kwa upande wa mashariki na Halmashauri za Kahama mji na Halmashauri ya nzega.kwa upande wa kaskazini imepakana na Halmashauri ya Msalala. Kwa upande wa magharibi imepakana na Halmashauri ya mbogwe na kwa upande wa kusini imepakana na wilaya ya Tabora
Eneo la kijeografia la Halmashauri ya Wilaya ya ushetu.
UKUAJI NA ONGEZEKO LA WATU
Kulingana na sensa ya idadi ya watu na makazi ya mwaka 2012 , Halmashauri ina jumla idadi ya watu 273,075 (138,846 kike; 134229 kiume), hata hivyo kundi la watu wenye nguvu kazi kwa ajili ya kufanya kazi na kusaidia kuinua uchumi wa nchi ni wakazi wapatao 183,411. kundi lwa watu ambao ni tegemezi ni jumla ya idadi ya wakazi wapatao 89,892 ; hii ni pamoja na wazee na watoto.
WASTANI WA PATO LA MWANANCHI
wastani wa Kipato cha kila mkazi wa Halmashauri ni takriban shilingi 530,000 / = (Hii ni sawa na shilingi 1,452 / = kwa kila Mkazi kwa siku) kutokana na sensa ya taifa ya watu na makazi ya mwaka 2012. kasi ya ukuaji huu unatokana na ukuaji wa kata za Ulowa, Ushetu na Bulungwa ambazo hushughulika na na shughuli za kilimo kama vile, pamba tumbaku na uzalishaji wa mazao ya chakula
SHUGHULI ZA KISIASA
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ina ina jimbo 1 la uwakilishi wa Wananchi. Halmashauri ina kata 20 za uwakilishi. na Mbunge mmoja wa kuchaguliwa . Madiwani wa kuteuliwa kwa viti maalumu vya wanawake ni 7 hivyo kufanya jumla ya Madiwani 27 na Mbunge 1.
Eneo na idadi ya watu kwa kata
Tarafa
|
|
Kata
|
Eneo
hekta |
Idadi ya watu ( Sensa of 2012)
|
|||
Household
|
Males
|
Females
|
Total
|
||||
Dakama
|
1
|
Chona
|
19,250.70
|
2971
|
8882
|
9599
|
18481
|
|
2
|
Chambo
|
23,162.20
|
2370
|
7084
|
7432
|
14516
|
|
3
|
Ukune
|
10,135.00
|
2243
|
5693
|
6024
|
11717
|
|
4
|
Mpunze
|
7,982.40
|
1573
|
4576
|
4762
|
9338
|
|
5
|
Igunda
|
6,068.70
|
1235
|
3182
|
3415
|
6597
|
|
6
|
Mapamba
|
8,567.00
|
960
|
3072
|
3201
|
6273
|
|
7
|
Kisuke
|
4342.12
|
1042
|
2288
|
2412
|
4700
|
|
8
|
Kinamapula
|
8,245.00
|
2105
|
6149
|
6546
|
12695
|
|
9
|
Bukomela
|
9,833.00
|
978
|
3220
|
3272
|
6492
|
|
10
|
Sabasabini
|
9,208.20
|
1794
|
5702
|
5861
|
11563
|
|
11
|
Idahina
|
35,601.30
|
3502
|
11912
|
12025
|
23937
|
|
12
|
Igwamanoni
|
20,994.40
|
2076
|
7245
|
7656
|
14901
|
Mweli
|
13
|
Uyogo
|
19,434.10
|
2315
|
7407
|
7884
|
15291
|
|
14
|
Ulowa
|
37,226.60
|
3282
|
9780
|
9450
|
19230
|
|
15
|
Ushetu
|
29,875.80
|
2708
|
8728
|
8810
|
17538
|
|
16
|
Ubagwe
|
18,456.00
|
2535
|
8362
|
8212
|
16574
|
|
17
|
Bulungwa
|
31,345.00
|
3941
|
12090
|
12552
|
24642
|
|
18
|
Nyankende
|
27,215.00
|
2208
|
7113
|
7402
|
14515
|
|
19
|
Ulewe
|
101,028.00
|
2832
|
8875
|
9433
|
18308
|
|
20
|
Nyamilangano
|
4,700.82
|
1,202
|
2780
|
2987
|
5697
|
Jumla
|
847,694.20
|
43,503
|
134229
|
138846
|
273075
|
JIOGRAFIA: HALI YA HEWA NA UOTO WA ASILI
MVUA
kwa ujumla kuna mvua zisizo za uhakika. Hata hivyo, mvua za masika hotofautiana Msimu kwa msimu, wastani wa mvua ni kati ya 750mm na 1,030 mm kwa mwaka. mvua hudumu kwa kunyesha takribani miezi mitano (5) kwa mwaka, kutoka mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi Mei na huwa nyingi kwa kipindi cha wiki mbili hadi mwezi mmoja kati ya Kipindi cha mwezi januari hadi febuari katika mwaka.
JOTO
joto huwa kiasi kwa kipindi cha mwaka mzima; wastani wa joto kila siku huwa ni kuanzia ° 21-26 ° C, Miezi ya Agosti na Septemba ndio miezi ya joto la juu kiasi. na hupungua baada ya kipindi hicho,Wastani wa joto kaatika sehemu zote za Wilaya hufanana.
HALI YA UNYEVU UNYEVU
Unyevu unyevu ni wastani wa 79% kwa mwaka. pamoja na tofauti ndogo katika mwaka huo; wakati wa msimu wa mvua kiwango huwa ni kati ya 80% na 85% na chini wakati wa kiangazi. kila mwezi spidi kasi ya upepo inaonekana kuwa tofauti kidogo- wastani wa spidi ya 0.9m kwa saa, wakati wa msimu wa mvua upepo hupungua kasi kuliko kipindi cha kiangazi. mara kwa mara kutokea kuhusishwa na rainstorms, hasa wakati wa msimu wa mvua
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa