Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo vinatolewa kwa wakati bila ucheleweshaji, ili kuwawezesha wananchi kuendesha shughuli zao halali kwa utulivu na bila bugudha.
Akizungumza kwenye Kongamano la wafanyabiashara Ndogondogo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu huyo wa Mkoa, RC Mhita amesema kuwa ucheleweshaji wa vitambulisho hivyo unakwamisha juhudi za kujenga mazingira rafiki ya biashara mkoani humo, hasa kwa wafanyabiashara wadogo wanaotegemea biashara zao za kila siku kwa maisha yao.
“Vitambulisho hivi vinapaswa kuwafikia walengwa kwa wakati. Tukichelewesha tunawapunguzia fursa za kiuchumi. Ninataka kuona kila mfanyabiashara anayestahili anapatiwa kitambulisho bila urasimu,” alisema RC Mhita.Katika hatua nyingine,
Mkuu huyo wa Mkoa ameridhia matumizi ya Soko la Ibinzamata kama gulio kwa siku moja kwa wiki, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuhamasisha biashara na kuwapa fursa wakazi wa maeneo hayo kufanya shughuli za kiuchumi kwa urahisi.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha uchumi wa wananchi wa maeneo ya pembezoni, sambamba na kupunguza msongamano katika masoko makuu ya mjini.RC Mhita amewataka viongozi wa halmashauri na wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara ili kuhakikisha fursa zilizopo zinawanufaisha wananchi wengi zaidi.
Mifuko hiyo imekamatwa kupitia kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Mkoa ili kuendelea na zoezi lililoanza Mwezi Oktoba mwaka jana 2018 lenye lengo la kuwakamata wahujumu uchumi Mkoani hapa.
Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2018 Mkoani Shinyanga katika kijiji cha Wishiteleja, Wilayani Kishapu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa