Na. Paul Kasembo, KISHAPU.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kishapu imefanya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ambao wamechaguliwa kupitia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba, 2024 huku msisitizo mkubwa ukiwa ni kwenda kuwatumikia wananchi wao bila kuweka Itikadi za vyama vyao na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Serikali za Mitaa.
Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Kishapu yametekelezwa na Wataalam kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Kampasi ya Shinyanga kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Ujio wa mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha aliyotoa tarehe 29 Novemba, 2024 wakati wa hafla ya uapisho wa Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wao iliyofanyika Manispaa ya Shinyanga ambapo alipowaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Shinyanga kuhakikisha wanawapatia mafunzo elekezi kabla ya Desemba, 2024.
Picha ikimuonesha ndugu Mohamed Kasinyo, mmoja kati ya wawezeshaji wa mafunzo akielezea jambo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa