Ukitaka kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii ili upate kitambulisho kitakachokuwezesha kutibiwa katika vituo vya kutolea huduma ya Afya, yaani Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali kwa mwaka mzima bila malipo, fuata hatua chache zifuatazo:-
1. Nenda kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata mahali unapoishi au kituo cha Afya chochote kilichopo karibu uulizie Afisa mwandikishaji wa CHF
2. Uwe na sh. 30,000/= kwa ajili ya kukuwezesha kujiandikisha wewe na familia yako yaani wewe na mke / mume wako na wategemezi au watoto 4 hivyo kufanya watu sita kwa familia / kaya moja.
3. Wakati wa kujiandikisha kwa Afisa mwandikishaji, utachukuliwa picha yako pamoja na wategemezi wote watano yaani mke / mume na wategemezi / watoto. Zoezi lote la uandikishaji na kupiga picha ni bure.
4. Kila mmoja atapata kitambulisho cha kwake yaani vitambulisho 6 kwenye familia moja
7. Hakikisha unaondoka na kitambulisho chako pamoja na vitambulisho vya kila mmoja katika familia yako.
8. Kila mmoja atatakiwa kwenda na kitambulisho chake katika kituo cha Afya kila atakapohitaji huduma ya Afya.
9. Muda wa matumizi ya kitambulisho hicho ni mwaka mmoja tangu siku uliyojiandikisha. Baada ya mwaka utatakiwa kufuata utaratibu huu kwa kulipa tena sh. 30,000/=
10. Kumbuka mfumo wa matibabu unaanzia ngazi ya Zahanati au Kituo cha Afya mahali ulipo hadi Hospitali ya Rufaa.
11. Huduma hii inapatikana katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.
"OKOA GHARAMA YA MATIBABU WEWE NA KAYA YAKO ISIYOZIDI WATU SITA KWA MWAKA MZIMA KWA SHILINGI 30,000/- TU"
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa