• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MHITA APONGEZA UONGOZI MPYA WA KANISA LA WASABATO NGBF MKOANI SHINYANGA.

Posted on: November 7th, 2025

Na Johnson James, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita leo Novemba 7,2025 amekutana na kupongeza uongozi mpya wa Kanisa la Wasabato la Nyanza Gold Belt Field (NGBF) waliofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha rasmi baada ya kuchaguliwa kuongoza kanisa hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Katika salamu zake, Mhe. Mhita aliwapongeza viongozi hao kwa dhamana waliyopewa na waumini wao, akiwataka kuwaongoza kwa hekima, maadili na uadilifu mkubwa. Alisisitiza kuwa uongozi wao unapaswa kuacha alama ya mshikamano, upendo na amani miongoni mwa waumini wao na jamii kwa ujumla.

“Ni matarajio yangu kwamba mtaendelea kuwa sehemu ya kuhakikisha jamii inakuwa imara kiroho na kijamii. Mkawe kielelezo chema kwa waumini wenu na jamii,” alisema RC Mhita.

Aidha, alibainisha kuwa Mkoa wa Shinyanga uko salama na shughuli za wananchi zinaendelea kama kawaida, huku akisisitiza kuwa maeneo yaliyowahi kuwa na changamoto za kiusalama kama Wilaya ya Kahama sasa yameimarishiwa ulinzi kwa ushirikiano na vyombo vya dola ili kuhakikisha ustawi wa kiuchumi unaendelea.

Viongozi waliochaguliwa  kuongoza NGBF kwa miaka mitano ni Mch. Shukrani Mutaki Askofu Mkuu, NGBF, Mch. Joshua Mbwambo Katibu Mkuu, NGBF, ELD. Padon Kikiwa Mhazini Mkuu, NGBF

Kwa upande wake, Mch. Joshua Mbwambo ambaye ni Katibu Mkuu wa NGBF, alitoa shukrani kwa Mkuu wa Mkoa kwa ukaribisho na ushirikiano aliouonesha kwa viongozi wa dini.  

“Tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kutupokea na kutupa maneno ya kututia moyo. Tunaahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali na kuwa sehemu ya kuhimiza maadili mema, amani na maendeleo miongoni mwa waumini na jamii ya Shinyanga,” alisema Mch. Mbwambo.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA

    November 13, 2025
  • RC MHITA AKUTANA NA MSANII BANDO MC, APONGEZA JUHUDI ZA KUSAIDIA VIJANA SHINYANGA

    November 11, 2025
  • RC MHITA APONGEZA UONGOZI MPYA WA KANISA LA WASABATO NGBF MKOANI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • WANAFUNZI 29,193 KUFANYA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • Angalia zote

Video

RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA

    Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa