• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Prof. Ndalichako - Mnaosema mil. 20 haitoshi kujenga darasa njooni Shinyanga kujifunza"

Posted on: November 10th, 2019

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameyasema hayo leo tarehe 10/11/2019 katika hafla ya kupokea vyumba vinne vya madarasa kutoka kwa umoja wa Wake wa Viongozi - New Millenium Women Group, katika shule ya msingi Buhangija vilivyojengwa kwa shilingi milioni 16.4 kila chumba chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

"Wengine wakipewa fedha hiyo wanasema haitoshi, lakini hapa imetosha na kubaki, nawapongeza sana. Nawasihi wale wanaosema mil. 20 haitoshi kujenga darasa waje Shinyanga kujifunza" 

Amewapongeza na kuwashukuru Wake wa Viongozi kwa kazi hiyo ya ujenzi wa madarasa na kusema kuwa wamefanya kazi ya kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Serikali ya awamu ya tano kwani Serikali inafanya kazi kubwa lakini pia mahitaji ni makubwa.

Aidha, amewasisitiza Watanzania wote kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watoto wenye ulemavu wa namna yoyote, kwani wana haki ya kupata elimu na kutimiza ndoto zao.

Akikabidhi madarasa hayo pamoja na matundu 10 ya vyoo, mlezi wa umoja wa wake wa viongozi Mama Mary Majaliwa ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kusimamia vizuri ujenzi huo na kuongeza umoja huo unaongeza sh. Mil 3.6 kwa ajili ya madawati.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela amesema, Mkoa ulipokea sh. Mil. 92 iliyotolewa na Umoja huo kwa awamu tatu na kukamilisha vyumba vyote vinne vya madarasa kwa sh. mil. 65.8 pamoja na matundu 10 ya vyoo yanayotarajiwa kukamilika mwezi ujao kwa gharama ya sh. mil .26.2

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ametoa shukrani za dhati kwa umoja huo wake wa Viongozi na kuwaomba waendelee kuguswa kuwasaidia watoto hao wa shule ya msingi Buhangija ambayo ni shule inayojumuisha na watoto wenye mahitaji maalum.




Matangazo

  • Matokeo ya kidato cha Sita mwaka 2019 July 11, 2019
  • Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Shinyanga May 07, 2019
  • Uzinduzi wa Utoaji wa Chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi April 20, 2018
  • Ziara ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani Shinyanga July 05, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Wafungwa 74 Shinyanga waachiwa kwa msamaha wa Rais Magufuli

    December 10, 2019
  • Waziri Jafo aridhishwa na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga

    December 07, 2019
  • Wananchi watakiwa kukaa mbali na maeneo ya Kambi za Jeshi kuepuka madhara

    December 04, 2019
  • RC Telack apiga marufuku bidhaa za vyakula kuwekwa juani

    December 04, 2019
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Hati ya Mshahara

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa