• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Serikali yafungia shughuli za Kiwanda cha Punda

Posted on: June 7th, 2018

Serikali imeuagiza uongozi wa kiwanda cha kuchinja Punda Mkoani Shinyanga kusimamisha shughuli zake hadi hapo watakapotekeleza sheria na taratibu za uendeshaji wa kiwanda ikiwemo kuweka mifumo iliyoelekezwa ya kuteketekeza taka ngumu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola ametoa agizo hilo wakati akikagua kiwanda hicho katika ziara yake ya siku moja Mkoani hapa tarehe 06/06/2018.

Mhe. Lugola ametoa siku 2 kwa kiwanda hicho, kuondoa mizoga na uchafu wote eneo la kiwanda pamoja na kushughulikia mizoga hiyo kwa namna bora inayotakiwa, hadi hapo Baraza la Taifa la Uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) litakapofanya uhakiki na kuridhia kuendelea kwa shughuli kiwandani hapo.

Katika ziara hiyo imebainika kuwa, kiwanda kimekaidi maagizo ya Manispaa ya Shinyanga ya kuacha kuchoma mifupa na uchafu wa matumbo katika eneo la kiwanda licha ya kuagizwa kwa maandishi tangu mwezi Machi mwaka huu.

"Wamekuwa na mifumo duni isiyokidhi matakwa ya kimazingira, Serikali ya Rais Magufuli haimuogopi Mwekezaji anayevunja sheria na kukaidi maagizo ya Serikali" amesema Mhe. Lugola.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bw. Geoffrey Mwangulumbi kuhakikisha mitaro inayotoka kwenye machinjio ya Manispaa iliyopo katika eneo la Nguzo Nane, pamoja na Mitaro mingine yote ya aina hiyo, inazibuliwa na kusafishwa ndani ya wiki moja ili kuondoa harufu mbaya eneo hilo.

Matangazo

  • Matokeo ya kidato cha nne na QT 2018 January 24, 2019
  • Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Shinyanga August 17, 2018
  • Uzinduzi wa Utoaji wa Chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi April 20, 2018
  • Ziara ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani Shinyanga July 05, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Matukio katika picha, ziara ya Mhe. Balozi Seif Ally Iddi Mkoani Shinyanga

    February 13, 2019
  • Shinyanga yapata magari yenye thamani ya sh. mil 189 kwa ajili ya shughuli za UKIMWI

    February 07, 2019
  • Ofisi za RC na DC zisiwe mahakama

    February 02, 2019
  • Wadau watoe elimu kuwazuia vijana kufanya ngono, siyo matumizi ya kondomu

    February 01, 2019
  • Angalia zote

Video

MAKABIDHIANO YA MWENGE WA UHURU 2018 MKOANI SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Hati ya Mshahara

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa