Na. Shinyanga RS.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu ameitaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga kuboresha Sekta kwa kutoa haki kwa wakati, kulinda amani na usalama kwa maendeleo ya Taifa hili, huku akisisitiza kuboreshwa kwa mnyororo wa utoaji wa haki jinai sanjari na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na weledi.
Dkt. Kazungu ameyasema haya leo tarehe 16/3/2024 wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Jengo hili lililopo Manispaa ya Shinyanga halfa ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali na Dini, ambapo pamoja na maelekezo haya Dkt. Kazungu pia amesema uzinduzi wa jengo hili unawakilisha majengo mengine (5) yaliyokamilika likiwemo la Ilala, Mkoa wa Pwani, Manyara, Katavi na Mkoa wa Rukwa.
"Niwatake Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Shinyanga kuboresha Sekta hii kwa kutoa haki kwa wakati, kulinda amani na usalama kwa maendeleo ya Taifa hili sanjari na kuboresha mnyororo wa utoaji wa Haki Jinai huku mkizingatia maadili ya kazi zenu na weledi katila kuwatumikia wananchi wetu," amesema Dkt. Kazungu.
Kwa upande wake Ndg. Sylvester Mwakitali ambaye ni Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa, muundo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka unaelekezq kuwepo kwa Ofisi za Mashtaka katika Mikoa yote na Wilaya zote. Hadi sasa zipo Ofisi katika Mikoa yote ya Kiserikali pamoja na mikoa minne ya Kimashtaka hivyo kufanya kuwa na jumla ya Ofisi 30 nq zote zinafanya kazi.
Akitoa salamu za Serikali Mhe. Joseph Mkude - DC KIshapu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya Bil. 2 kujenga jengo hili la Ofisi ambapo kukamilika kwake kunakwenda kusogeza na kuboresha huduma kwa jamii pamoja na kuimarisha mnyororo mzima wa utoaji haki jinai.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni Taasisi iliundwa mwaka 2018 kufuatia mabadiliko ya Muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambapo iliyokuwa Divisheni ya Mashtaka chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuwa huru na Mamlaka kamili.
HABARI PICHA
Dkt. Khatibu Kazungu akielezea jambo wakati wa hafla
Mhe. Joseph Mkude, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa