Na. Shinyanga RS.
SERIKALI imesaini Mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Kahama - Bulyanhulu Jct - Kakola (KM 73) kwa kiwanho cha Lami ili kufungua fursa za kiuchumi katika nyanja ya kilimo, madini na misitu katika kati ya Mkoa wa Shinyanga, Geita, Kagera na Kigoma.
Mkataba huu umesainiwa kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya Tzs. Bil. 101.2 kwa ufadhili wa Barrick Tanzania Mining Companies (BTMCs) na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza katika utiaji saini wa kandarasi hii, Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa uhitaji wa barabara hii umekuwa ni muda mrefu sana na kilio cha walio wengi kulingana na umuhimu wake.
Na sasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikia kilio hiki, kwa ushirikiano wa wawekezaji wa ndani ya Nchi ikiwemo Barrick ametoa kibali ili barabara hii ianze kujengwa kwa kiwango cha lami.
"Niwashukuru Barrick kwa ushirikiano ambao wanatupatia na sasa ujenzi wa barabara ya KM 73 inaanza kujengwa na mkandarasi mbobezi sana ambapo ataijenga kwa kipindi cha miezi 27 na siyo zaidi ya hapo," amesema Mhe. Bashungwa.
Aidha Mhe. Bashungwa amesema pia Mhe. Rais ameelekeza Wizara ya Ujenzi kuanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kutoka Iloginhandi Mtakuja (KM 57.4) ambayo ni barabara ya kiuchumi na inaunganisha Mkoa wa Shinyanga na Geita.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa