Shughuli kuu ya wakazi wa Shinyanga zaidi ya asilimia 80 ni Kilimo.
Kilimo kina nafasi muhimu katika kuajiri wananchi wengi, upatikanaji wa chakula, mauzo ya mazao ndani na nje ya nchi na malighafi za viwanda. Pia ni chanzo cha kipato kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Eneo linalofaa kwa Kilimo
Mkoa una eneo la kilometa za mraba 18,555 sawa na hekta 1,855,500 ambapo hekta 1,220,090 zinafaa kwa kilimo.
Eneo la kila Halmashauri, Eneo linalofaa na linalolimwa
Halmashauri
|
Eneo la Halmashauri (ha.) |
Eneo linalofaa kwa Kilimo (ha.) |
Eneo lililolimwa 2015/2016 (ha.) |
Asilimia ya Eneo lililolimwa |
Kahama (M)
|
151,500 |
71,874 |
45,100 |
63 |
Msalala
|
263,500 |
210,000 |
144683 |
69 |
Ushetu
|
531,100 |
395,011 |
282580 |
72 |
Kishapu
|
433,400 |
319,200 |
167985 |
53 |
Shinyanga (W)
|
421,200 |
171,375 |
105,777 |
62 |
Shinyanga (M)
|
54,800 |
52,630 |
15,210 |
29 |
Jumla Kuu
|
1,855,500 |
1,220,090 |
761,335 |
62 |
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga
Kilimo cha Mazao ya Chakula
Mazao makuu ya chakula yanayolimwa katika Mkoa wa Shinyanga ni mtama, uwele, mpunga, mahindi, viazi vitamu na mihogo.
Kilimo cha Mazao ya Biashara
Mazao makuu ya biashara ni pamba, tumbaku, alizeti, dengu, karanga, choroko na ufuta.
Kilimo cha katani kilianza mwaka 2011 kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la OXFAM GB. Hadi sasa kuna wananchi 43 na vikundi 5 ambavyo vimelima ekari 137 za katani. Wakulima hawa wanauza nyuzi za katani kwa kampuni ya Tanga Katani Limited kwa bei ya sh.1200 kwa kilo.
Kilimo cha Umwagiliaji
Eneo linalofaa kwa umwagiliaji katika Mkoa ni hekta 221,896. Eneo linalomwagiliwa ni hekta 4,899 sawa na asilimia 2.2 ya eneo linalofaa kwa umwagiliaji.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa