Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Mbosso Khan leo Agosti 22, 2025 ametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ikiwa ni sehemu ya kuonesha mshikamano na kuthamini mchango wa serikali katika kukuza sekta ya sanaa na burudani nchini.
Akiwa ofisini kwake Mhe. Mboni Mhita amempongeza Mbosso kwa kuwa balozi mzuri wa vijana na kutumia kipaji chake kuelimisha, kuburudisha na kuhamasisha jamii. Aidha, amemkaribisha kushirikiana na Mkoa wa Shinyanga katika shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo.
RC Mhita pia alisisitiza kuwa Mkoa wa Shinyanga unaendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana na wasanii, kwa kutambua kuwa sanaa ni fursa muhimu ya ajira na kipato kwa vijana, sambamba na kusaidia katika kukuza utalii wa ndani.
Katika mazungumzo yao, Mbosso ameonesha kufurahishwa na maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa mkoani humo, hususan kwenye sekta ya vijana, michezo na sanaa. Amesema wasanii wana jukumu la kushirikiana na viongozi kuhamasisha amani, mshikamano na maendeleo ya kijamii.
Mbosso yupo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kushiriki shughuli za kijamii pamoja na kutoa burudani kwa wakazi wa mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kisanaa inayolenga kuungana na mashabiki wake na kutoa mchango katika maendeleo ya jamii.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa