Almasi yenye ukubwa wa karati 521 imepatikana Mkoani Shinyanga kutoka kwa mchimbaji mdogo na kuwa Almasi ya mfano Nchini Tanzania tangu kuanza kuchimbwa madini hayo.
Akitoa taarifa hiyo Ofisini kwake mbele ya waandishi wa Habari leo tarehe 30 Aprili, 2019, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema almasi hiyo itauzwa ndani ya nchi ili kodi itakayopatikana ibaki katika Mkoa wa Shinyanga na nchini hapa.
" Ni almasi kubwa ambayo haijawahi kupatikana kwenye Mkoa wetu hususani katika Mgodi wa Mwadui ambao ni wa zamani sana, ambao uliwahi kupata karati 300-400, katika kipindi cha miaka 87 ni fahari kubwa kwa Mkoa wetu" amesema Mhe. Telack.
Mhe. Telack ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara wote wa Almasi kuja kununua katika Mkoa wa Shinyanga ambapo tayari soko la madini katika Wilaya ya Kahama linaendelea vizuri wakati soko jingine la madini litafunguliwa katika Wilaya ya Shinyanga hapo tarehe 3 Mei, 2019.
Aidha, ametoa wito kwa wafanyabiashara wote ndani ya Mkoa kuendelea kutumia masoko yaliyoandaliwa kwa ajili ya uuzaji wa madini, waache kununua katika maeneo yasiyo rasmi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa