Askofu wa jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu ameyasema hayo leo tarehe 14 Novemba, 2019 kwenye misa ya shukrani ya Jubilee ya miaka 25 ya upadri iliyofanyika katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma, Parokia ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga.
Akitoa salamu za shukrani kwa Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Harrison Mwakyembe pamoja na wote walioshiriki kuadhimisha Jubilee hiyo, Sangu amesema kuwa, Serikali la awamu ya tano imefanya mambo makubwa ambayo kwa mtu mwenye akili timamu anapaswa kupongeza.
"Mtu ambaye hajaona Rais Magufuli amefanya nini kwa kipindi cha miaka minne achuguzwe akili, kama ana akili timamu basi ana wivu" amesema Askofu Sangu.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanataaluma mbalimbali na wapiga kura kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa amani na utulivu, kwa ajili ya ustawi wa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, akimkaribisha Mgeni rasmi amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuombea amani ya Nchi na kuwaomba waendelee na kazi hiyo kubwa.
"Shinyanga kuna amani, kwani mmekuwa mkifanya kazi kubwa kuombea amani ya Taifa letu ndiyo sababu tupo hapa tunasherekea kwa amani na utulivu, naomba endeleeni kuombea amani ili tufanye kazi kwa amani na tupate chakula cha kutosha" Amesisitiza Mhe. Telack.
Aidha, Telack amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 24 Novemba, 2019 ili wawachague viongozi wanaowafaa.
Misa hiyo imehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mama Anna Makinda, Spika wa Bunge Mstaafu, Mhe. Nape Nnauye Mbunge wa Jimbo la Mtama - Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Viongozi waandamizi wa Mkoa na Wilaya ya Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa