Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa wake wa Viongozi nchini akitoa neno katika hafla fupi kwenye ukumbi wa shule ya msingi Buhangija, ambapo ameelezea historia na shughuli zinazofanywa na katika kusaidia jamii na kusema kuwa wameguswa sana na watoto wenye ulemavu lengo lililowafanya kuamua kujenga madarasa hayo
Mama Kighoma Malima ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wake wa Viongozi, akiwatambulisha wakina mama waliopo katika Umoja huo kwenye ukumbi wa shule ya msingi Buhangija
Mkuu wa shule ya msingi Buhangija Bw. Selemani Kipanya akitoa taarifa ya shule hiyo na kuwashukuru akina mama kwa msaada walioutoa
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela (kulia), akitoa maelezo kwa akina mama Wake wa Viongozi kuhusu ujenzi wa matundu ya vyoo kanika eneo la ujenzi wa vyoo hivyo ambapo amewahakikishia vitakamilika baada ya muda mfupi
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, (katikati) na Mama Malima (wa tatu kutoka kulia), wakicheza na kufurahi na watoto wa shule ya msingi Buhangija kabla ya kukabidhi madarasa kwa Waziri Ndalichako, jana tarehe 10/11/2019
Akina mama Wake wa Viongozi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, pamoja na watoto wa shule ya msingi Buhangija katika picha ya pamoja hapo jana baada ya kukabidhiwa madarasa manne yaliyojengwa na akina mama hao
Mama Mary Majaliwa Mke wa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitoa neno baada ya kumkabidhi madarasa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Joyce Ndalichako hapo jana tarehe 10/11/2019 katika shule ya msingi Buhangija
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Buhangija, wakicheza kwa furaha mbele ya madarasa yaliyojengwa na umoja wa wake wa Viongozi na kukabidhiwa kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia hapo jana tarehe 10/11/2019
Kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Mama Tunu Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, Mama Mary majaliwa na Wake wengine wa Viongozi wakiangalia moja ya chumba cha darasa kati ya vyumba vinne vilivyojengwa na Umoja wa Wake wa Viongozi jana tarehe 10/11/2019 katika shule ya msingi Buhangija
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (kushoto) akimuongoza Mama Mary Majaliwa (katikati) na Mama Tunu Pinda (kulia) kuelekea kwenye darasa mojawapo katika shule ya msingi Buhangija
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack (mbele kushoto) akicheza kwa furaha pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (wa tatu kulia),Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga (wa pili kulia) na Wake wa Viongozi, mbele ya chumba cha darasa kati ya vinne vilivyojengwa na Wake wa Viongozi shule ya msingi Buhangija
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (mwenye skafu) akikata utepe kuonesha kupokea vyumba vinne vya madarasa kutoka kwa Umoja wa Wake wa Viongozi katika shule ya msingi Buhangija
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Buhangija
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakipokea salamu kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi buhangija baada ya kuwasili katika eneo hilo jana
Viongozi wa Mkoa na Wilaya, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wake wa Viongozi wakiimba kwa pamoja na watoto wa shule ya msingi Buhangija (hawapo pichani)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akivishwa skafu na Skauti baada ya kuwasili eneo la shule ya msingi Buhangija
Mama Mary Majaliwa alipokuwa akiwasili katika eneo la shule ya msingi Buhangija hapo jana
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa Bw. Albert Msovela mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Buhangija
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko mara baada ya kuwasili katika shule ya msingi Buhangija
Wake wa Viongozi wakiongozwa na Mama Mary Majaliwa pamoja na Waziri Ndalichako kutoa huduma ya chakula kwa watoto wa shule ya msingi Buhangija baada ya kukabidhi madarasa
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa