Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Balozi Seif All Idd amewaahidi wananchi wa Wilaya ya Kahama kuhakikisha mchakato wa ujenzi wa barabara ya Kahama – Geita kwa kiwango cha lami unakamilika na barabara hiyo kujengwa.
Mhe. Balozi ametoa ahadi hiyo leo katika kijiji cha Buganzo, kata ya Ntobo, Wilaya ya Kahama wakati akizungumza na wananchi kwenye ziara yake Mkoani Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Msalala lililopo katika Wilaya ya Kahama Mhe. Ezekiel Maige akitoa salamu kwa Mhe. Balozi amemuomba kusaidia kukamilisha mchakato wa taratibu za Mkandarasi.
Mhe. Maige amesema barabara hiyo inayounganisha Mikoa ya Shinyanga na Geita ilishatengewa bajeti ya sh. Bilioni 22 isipokuwa, taratibu za Mkandarasi hazijakamilika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemueleza Mhe. Balozi kuwa, Serikali ya awamu ya Tano imefanya mambo mengi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa