Na. Paul Kasembo, SHY RS.
AFISA Hesabu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Evaline Msangi mapema leo tarehe 27 Agosti, 2024 amefika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Dome, Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga na kuboresha taarifa zake huku akitoa hamasa kwa wale ambao bado hawajafika kwenye vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwenda ili wahudumiwe kabla muda uliopangwa haujafikia mwisho saa 12:00 jioni ya leo Jumanne.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura kwa Mkoa wa Shinyanga ulianza tarehe 21 Agosti, 2024 utakamilika rasmi leo tarehe 27 Agosti, 2024 huku wito ukiendelea kutolewa kwa wananchi kujitokeza zaidi ili kutumia muda uliobakia waweze kupata huduma.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa