Na. Paul Kasembo, SHY RS.
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema kuwa Serikali kupitia Mguko wa Mawasiliano kwa wote imegharamia zaidi ya shilingi Bilioni 4 ambao zitatumika kuimarisha mawasiliano mkoani Shinyanga kwa kujenga minara 30 katika Kata 29 vyenye jumla ya vijiji 83 ambapo takribani wakazi 421, 259 watanufaika huku akisisitiza matumizi sahihi na yenye faida na siyo vinginevyo.
Mhe. Nape ameyasema haya tarehe 19 Julai, 2024 wakati wa wasilisho la Taasisi mbalimbali lililofanyika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi, kampuni za simu na wadau wa mawasiliano mkoani shinyanga.
"Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na mawasiliano ya simu, ambapo kwa mkoa huu wa shinyanga Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ikiwakilisha Serikali inayapatia makampuni ya simu kujenga minara 30 katika Kata 29 ambapo ndani yake kuna vijiji 83 na hivyo kuwanufaisha wakazi 421, 259 wa Mkoa wa Shinyanga, hili ni jambo kubwa sana na lenye kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha mawasiliano kwa Wanashinyanga," amesema Mhe. Nape.
Kwa upande wake RC Macha amempongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha mawasiliano kwa wanashinyanga na Tanzania kwa ujumla jambo ambalo linaimarisha ulinzi, kuongeza uchumi wetu.
Akiwa Shinyanga Mhe. Nape amezindua mnara wa Kampuni ya Halotel uliojengwa katika Kata ya Busangwa ambapo Serikali imetoa fedha zake za ruzuku shilingi Mil. 145 ambapo wakazi zaidi ya 12,100 kutoka vijiji vya Mwanima, Mwajipungira, Pambe na Busangwa vyote vya Wilaya ya Kishapu watanufaika.
Kisha amemalizia kwa kukagua na kupongeza ujenzi mzuri na bora wa mnara wa Kampuni ya Honora uliopo Kata ya Bukomela, Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu wenye uwezo wa 2G, 3G, 4G na 5G ambao utawanufaisha wakazi wa vijiji vitano (5) ikiwa ni zaidi ya lengo la awali la vijiji viwili (2) na kuwafikia wakazi zaidi ya 20 elfu.
HABARI PICHA
Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha
Mkurugenzi Mtendaji Mfuko wa Mawasiliano kwa wite Bi. Justina Mashiba
Mnara wa Honora Kata ya Bukomelo - Halmashauri ya Ushetu
Mnara wa Hatolel uliojengwa Kata ya Busangwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Picha ikionesha baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa hafla ya ufunguzi wa mnara wa Honora - Ushetu
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa