Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko amewataka wafanyakazi wa migodi nchini kuwa waadilifu ili kutoiweka nchi kwenye aibu ya sifa mbaya kwa wananchi wake.
Mhe. Biteko amesema baadhi ya Wawekezaji wanalalamika kuwa, Watanzania wamekuwa na mazoea ya uvivu na kuiba vitu vya Kampuni hali inayopelekea kutoaminiwa na hivyo kazi nyingi kupewa raia wa kigeni.
"Moja ya vitu vinavyotutia aibu ni baadhi ya wenzetu kuwa na mikono ya udokozi" Amesema Biteko na kusisitiza kuwa hata Wawekezaji wanasema.
Amewataka pia kuacha tabia ya uvivu na sababu nyingi zisizokuwa na maana hali inayosababisha kuzorotesha kazi za makampuni.
Amesema hali hiyo inachangia kuharibu sifa za hata vizazi vijavyo kushindwa kuaminiwa kutokana na wazazi kuwekeza katika uvivu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa